New Ads

computer solutiontricks

HOW TO HACK WHASTSAPP CHATS


KWANZA KABISA TUJIKUMBUSHE NINI MAANA YA UDUKUAJI (HACKING)
: UDUKUAJI (HACKING) NI KITENDO CHA KUCHUNGUZA, KUSOMA, KUCHUKUA AU KUBADILI TAARIFA ZA MTU MWINGINE KWENYE MTANDAO PASIPO RUHUSA AU IDHINI YA MUHUSIKA.


SASA TURUDI KWENYE SOMO LLETU LA LEO

KUZINDULIWA KWA MFUMO WA KUTUMIA MTANDAO WA WHATSAPP KWENYE COMPUTER YAANI (WHATSAPP WEB) KUMECHANGIA SANA NA KUCHOCHEA TATIZO LA UDUKUAJI WA TAARIFA KATIKA MTANDAO HUU, KWA SOMO LA TAREHE 21/3/2017 TULIJIFUNZA NAMNA YA KUUNGANISHA ACCOUNT YA WHATSAPP NA COMPUTER YAKO, KAMA ULIKOSA SOMO HILO SOMA HAPA    

SASA LEO TUNAENDA KUJIFUNZA NAMNA YA KUTAMBUA KAMA ACCOUNT YAKO YA WHATSAPP IMEDUKULIWA NA NAMNA YA KUMUONDOA MDUKUAJI

1: NAMNA YA KUTAMBUA KAMA ACCOUNT YAKO YA WHATSAPP IMEDUKULIWA AMA LA.

FUATA HATUA ZIFUATAZO

1: Ingia kwenye account yako ya whatsapp kwa kuclick app yako kama hivi

 

2:  Kisha baada ya hapo ikifunguka utatakiwa kuclick (kubofya) kwenye nukta tatu ambazo zipo upande wa kulia juu kabisa kama hivi


3: kisha baada ya hapo utatakiwa kubonyeza sehemu iliyoandikwa whatsapp web kama hivi:-


4: Endapo itakuja option au ujumbe kama huu ufuatao ujue na utambue kuwa account yako iko salama na haijadukuliwa (NOT HACKED)


5: Ila kama yamekuja  maandishi au message kama hiyo hapo chini basi ujue account yako imedukuliwa (HACKED) angalia picha hii:-

 
NAMNA YA KUJITOA KWA MDUKUAJI (HACKER) ILI ASIENDELEE KUDUKUA (HACK) ACCOUNT YAKO YA WHATSAPP

Kujitoam kwa mdukuaji (HACKER) ni rahisi sana kwani endapo umeikuta message / maandishi kama hayo hapo chini unachotakiwa kufanya ni kuBONYEZA MAANDISHI YALIYOANDIKWA " LOG OUT FROM ALL COMPUTER"  Kama inavyoonesha picha hapo chini:-

Sasa basi baada ya kubofya hapo utakua umejiondoa kwenye computer yake.
Ili kuthibitisha hilo tafadhali fuata step / hatua zote na mwisho ukikutana na ujumbe kama huu hapo chini basi utakua umejitoa kwa mdukuaji (HACKER)
Tahadhali: EWE NDUGU MSOMAJI WA MAKALA ZANGU UKURASA HUU (MDOPE BLOG) UNAKUFUNDISHA MBINU HIZI KWA LENGO LA KITAALUMA TU WALA SITAHUSIKA NA MAKOSA YOYOTE YATAKAYO JITOKEZA BAADA YA WEWE KUTUMIA TAALUMA HII KINYUME. IKUMBUKWE KUWA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO IPO A INAFANYA KAZI.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]