Blog designcomputer solutiontricks
MDOPE BLOG: Mafunzo ya blog Sehemu ya Kwanza: Blog ni nini?
Maana ya blog:
blog ni tovuti yenye maingizo yanayoitwa machapisho (posts) ambayo
huonekana katika kwa utaratibu wa kutangulia chapisho jipya kwanza na
kufuatiwa na machapisho ya nyuma. Kwa mfano kama juzi, jana na leo
umeandika machapisho na kuyachapa katika blog yako basi katika kurasa
yako ya mbele litaonekana kwanza chapisho la leo kisha la jana na kisha
la juzi. Blog huhusisha makala unazochapa (machapisho), viungo (links)
na maoni (comments) ya watembeleaji ili kuongeza maingiliano ya
kimawasiliano kati ya blog na watembeleaji blog hiyo. Kwa kawaida blog
huumbwa kwa programu maalum za kuchapishia.
Program za kublog:
ü Blogger (www.blogspot.com)
ü Wordpress (www.wordpress.com)
ü Drupal
ü Movable Type
ü TypePad
ü Livejournal
ü b2evolution
Mnyambuliko wa neno blog:
ü Kublog: kitendo cha kuandaa machapisho na kuyachapa katika blog
ü Mwanablog: mtu ambaye anaandika machapisho katika blog
ü Ulimwengu wa blogu: jumuiya/jamii/ ya wanablog na vinavyohusiana na blog katika mtandao
Hali ya mtandao kabla ya kuanza kwa blog:
Kuanzia mwaka 1989 ulipogunduliwa mtandao (Web 1.0) hadi 2004 mtandao
ulikuwa ni kama chombo cha kutolea habari tu. Wenye tovuti walikuwa
wakitoa habari walizonazo lakini hapakuwa na nafasi ya kumuwezesha
mtembeleaji kuweza kutoa mchango wake katika habari hizo ama kushiriki
kwa namna yeyote zaidi ya kusoma na kutazama tu. Hivyo tunaita kuwa
mtandao ulikuwa ni wa mazungumzo ya upande mmoja tu na kuacha upande wa
pili kuwa wasikilizaji.
Baadae katika maendeleo ya mtandao kulianza kuwa na maingiliano ambapo
ulianzishwa utaratibu wa kuweza kununua kupitia katika mtandao lakini
bado mtandao ulibaki kuwa ni wa upande mmoja kutoa taarifa na mwingine
kusikiliza.
Mwaka 2004 wakati wa mageuzi “rasmi” ya mtandao kutoka “Web 1.0” kuingia
“Web 2.0” (mtandao wa kijamii) yalifanya maudhui (contents) ya
mtembeleaji kuwa ni sehemu muhimu ya ulimwengu wa mtandao. Leo hii tuna
mtandao ambao unajumuisha mazungumzo ya pande mbili ambapo mtembeleaji
anaweza kushiriki kwa kuingiza mchango wake kwa mtindo wa maoni na njia
nyinginezo za mitandao ya kijamii. Hapa ndipo blog ilipozaliwa katika
ukamilifu wake tulionao sasa (Ikumbukwe kuwa blog ilikuwepo tangu miaka
ya 1990 lakini hapakuwa na maingiliano na mtembeleaji)
Kuzaliwa kwa Blog:
Awali blog ilianza miaka ya 1990 kama shajara (Diary) ya mtandaoni. Watu
binafsi walikuwa wakichapisha habari na matukio yao ya maisha ya kila
siku na kutoa mitazamo yao juu ya mambo tofauti wanayokutana nayo katika
maisha. Machapisho yalikuwa yakijipanga katika blog kwa kuanza na yale
ya karibuni zaidi kisha kufuata na yaliyopita ili kuleta maana zaidi kwa
msomaji.
Kutokana na maendeleo ya mtandao viliongezwa vitu vinavyowezesha kuwepo
na mazungumzo ya pande mbili na kumfanya mtembeleaji kuweza kutoa maoni
yake ama kuongeza kiuno katika blog ama tovuti nyingine kwenda katika
blog aliyosoma ili kuongeza mjadala zaidi katika mtandao
Hali ya blog kwa sasa:
Mtandao uimekuwa zaidi wa kijamii, blogs zimepata umaarufu mkubwa katika
mtandao. Leo, kuna blog zaidi ya milioni 100 na kila siku blog mpya
zinaingia katika ulimwengu wa blog kila siku. Blog zimekuwa ni zaidi ya
shajara za mtandaoni. Kwa kweli, wanablog wamekuwa sehemu muhimu ya
ulimwengu wa mtandaoni na nje ya mtandao na wanablog maarufu wamekuwa
wakileta athari kubwa katika ulimwengu wa siasa, biashara na jamii kwa
ujumla.
Mustakabali wa blog:
Ni suala lisilopingika kuwa wanablog wanaonekana kuwa na nguvu zaidi
katika siku zijazo na jamii na wafanya biashara wametambua uwezo wao wa
ushawishi katika kuvutia masoko na kubadili muelekeo wa jambo katika
jamii.
Kwa sasa kila mtu anaweza kuanzisha blog bure kabisa ilimradi uweze
kupata mtandao. Swali langu kwako ni je, unayo blog kwa sasa? Kama unayo
basi iweke katika kipengele cha maoni hapo chini. Kama hauna basi
tuambie kwa nini huoni umuhimu wa kuwa na blog yako.
No comments:
Post a Comment