New Ads

afya

AFYA: KUONDOA MADOA MEUSI USONI(FACIAL BLACK SPOTS)

MADOA MEUSI USONI(FACIAL BLACK SPOTS)

Madoa meusi (black spots) usoni ni jambo ambalo linawasumbua sana watu wengi na hupelekea mtu kutokujiamini na mara nyingine kujidharau. Hili tatizo husabaishwa na vitu tofauti,hivyo kujua chanzo cha tatizo ni muhimu sana.
Sababu zinazosababisha madoa meusi usoni ni kama ifuatavyo;

1.hyperpigmentation
Hili tatizo linatokea pale ngozi inapoharibiwa katika eneo fulani,hivyo husababisha ngozi kutengeneza ‘melanin’ nyingi na kusababisha eneo hilo kuonekana nyeusi kuliko nyingine.
2.homoni kutokuwa katika kiwango sahihi katika mwili(hormonal imbalances).
Pia hili husababisha madoa meusi usoni, na hili linaweza tokea wakati wa ujauzito,kwa watu wanaotumia vidonge vya uzazi wa mpango(control pills) na pia mwanamke anapoingia katika kipindi cha ukomo wa kuzaa(menopause).
3.kukaa juani kwa muda mrefu(excessive sun exposure).
Pia hii hutokea kwasababu mwili unaanza kutengeneza ‘melanin’ kwa wingi ili kuzuia kuharibiwa kwa ngozi na mionzi ya jua.
4.chunusi
pia hutokea kwa watu ambao wana tatizo la chunusi. Mara nyingi haya madoa meusi yanapotea baada ya muda fulani kupita,lakini muda mwingine inaweza ikawa ni ngumu kupotea yenyewe kutokana na aina hizo za chunusi.
Jinsi ya kuondoa madoa meusi ukiwa nyumabani
1.tumia limao(lemon).
Hakikisha unaosha uso wako vizuri kwa maji safi na sabuni inayofaa. Chukua limao na ulikate na kukamua juice yake. Tumia pamba au kitambaa safi kupaka hiyo juice ya limao sehemu yenye matatizo. Hakikisha unaacha kwa nusu saa kabla ya kuosha uso wako. Fanya hivi kwa muda wa wiki kadhaa utaona mabadiriko.
2.tumia juice ya aloe vera
Pia paka sehemu yenye madoa meusi mara mbili kwa siku. Fanya hivi kwa wiki kadhaa na utashuhudia mabadiriko makubwa.
3.asali na sukari
Changanya asali na sukari hii ya kawaida na ujifanyie ‘massage’ mara mbili kwa wiki. Hii husaidia kuondoa chembechembe za ngozi zilizokufa na kufanya ngozi mpya na hivyo kuondoa madoa meusi.
4 tumia matunda ambayo yana uwingi wa vitamin C na E
Matunda kama machungwa yana vtamin C ambavyo ni Antioxydant na pia hupunguza melanin isitengenezwe kwa wingi na hivyo kufanya ngozi isiwe na madoa meusi. Pia matunda ambayo yana vitamin E kwa wingi ni muhimu kuyatumia ,mfano Carrots.
5.pia tumia sunscreen cream.
Hizi cream huzuia mionzi ya jua ambayo ni chanzo mojawapo cha madoa meusi usoni, kwa hiyo hakikisha unatumia sunscreen cream kabla ya kutoka kwa ajili ya matembezi ya hapa na pale.
Pia ukiona madoa yako hayatoki unaweza ukamwona mtaalam wa ngozi kwa ajili ya ushauri na matibabu zaidi.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]