New Ads

academic

KISWAHILI: TAZAMA NAHAU ZAIDI YA 70 ZA KISWAHILI NA MAANA ZAKE



Imenukuliwa kutoka Gazeti la HABARILEO, Tanzania la Alhamisi,  Januari 8 - 14, 2015
                                       
 NA MWALIMU MDOPE @ 2016.


BASI MPENZI MSOMAJI WAWEZA KUWA MWANAFUNZI, MWALIMU AU HATA MUHITIMU. HIVYO KAMA ILIVYO ADA WIKI HII TATAANGAZIA NAHAU NA MAANA AZKE KATIKA LUGHA YETU YA KISWAHILI ZILIZOKUSANYWA KWA UWEREDI UKUMBWA SANA HIVYO TAZAMA HAPA,,,,,,, KWANI MDOPE COOOPERATION BLOG INAKUPA KILA UNACHOKIPENDA


  1. Amekula chumvi nyingi            -  Ameishi miaka mingi [lived a long life]
  2. Ahadi ni deni                           - Timiza ahadi yako [be trustworthy; keep your promise]
  3. Amewachukua wazee wake   -  Anawatunza vizuri wazazi wake [taking good care of parents]
  4. Amekuwa popo                      - Yu kigeugeu [ a turncoat]
  5. Amevaa miwani                      - Amelewa pombe [chakari] [inebriation, a drunkard]
  6. Amekuwa mwalimu                 - Yu msemaji sana  [a talkative person]
  7. Amemwaga unga                     - Amefukuzwa kazi [ dismissed from employment]
  8. Ana ulimu wa upanga               - Ana maneno makali  [biting words]
  9. Ameongezwa unga                  - Amepandishwa cheo [promoted]
  10. Agizia risasi                             - Piga risasi  [shoot!]
  11. Chemsha bongo                      - Fikiri kwa makini  [think analytically]
  12. Kuchungulia  kaburi                 - Kunusurika kifo   [saved from a worse fate]
  13. Fyata mkia                              - Nyamaza [keep silent]
  14. Fimbo zimemwota mgongoni    -Ana alama ya mapigo ya Fimbo mgongoni [birching scars on ones' back]
  15. Hamadi kibindoni                    - Akiba iliyopo kibindoni [savings for a rainy day]
  16. Hawapikiki chungu kimoja       -Hawapatani kamwe !  [always at loggerheads]
  17. Kupika majungu                      - Kufanya mkutano wa siri [conspire a secret meeting]
  18. Kumpiga [kumvika] kilemba cha ukoka   -  Kumsifu mtu kwa unafiki [kinafiki] [paying lip service]
  19. Kula mlungula                          - Kula rushwa [receiving a bribe]
  20. Kupelekwa miyomboni            - Kutiwa [kupelekwa] jandoni [performing circumcision]
  21. Kujipalia mkaa                         - Kujitia matatani [get yourself in trouble]
  22. Kumeza [zea] mate                  - Kutamani   [to crave for]
  23. Kumuuma mtu sikio                 - Kumnong'oneza mtu jambo la siri [tell a secret to someone]
  24. Kumpa nyama ya ulimi             -Kumdanganya mtu kwa maneno matamu [using wiles to tell lies]
  25. Kumchimba mtu                      - Kumpeleleza mtu siri yake  to dig one's secrets]
  26. Kutia chumvi  katika mazungumzo  -  Kuongea habari za uwongo [tell lies]
  27. Vunjika moyo                          -  Kata tamaa [give up]
  28. Yalimkata maini                       - Yalimtia uchungu  [emotional pain]
  29. Kujikosoa                               - Kujisahihisha  [correct your ways]
  30. Kutia utambi                            - Kuchochea ugomvi  [convince someone to fight]
  31. Kumeza maneno                      - Kutunza siri moyoni  [to keep a secret]
  32. Kula njama                              - Kufanya mkutano wa siri [to conspire a secret meeting]
  33. Kumkalia mtu kitako                - Kumsema/kumsengenya  [to talk about someone]
  34. Kupiga vijembe                        - Kumsema mtu kwa fumbo [use idioms to talk about someone]
  35. Kiinua mgongo                         - Malipo ya pongezi/uzeeni [pension]
  36. Kazi ya majungu                       - Kazi ya kumpatia mtu posho [hand to mouth existence]
  37. Kaza kamba                             - Usikate tamaa - [never give up!]
  38. Kumwonyesha mgongo             -  Kujificha - [to hide]
  39. Kuona cha mtema kuni             -  Kupata mateso [torture]
  40. Maneno ya uwani                     - Maneno yasiyo na maana/porojo  -  [hyperbole !]
  41. Mate ya fisi                              -  Kata tamaa kupita kiasi - [give up totally !]
  42. Mbiu ya Mgambo                     - Tangazo [advertisement]
  43. Mungu amemnyooshea kidole   - Mungu amemuadhibu -  [God's punishment]
  44. Mkubwa jalala                          - Kila  lawama hupitia kwa mkubwa - [The eldest is the Dumping ground!]
  45. Mkaa jikoni                               - Mvivu wa kutembea -  [a stay at home person]
  46. Mungu si Athumani                    - Mungu hapendelei [God is fair]
  47. Ndege mbaya                            - Bahati mbaya [bad luck]
  48. Paka mafuta kwa mgongo wa chupa - Danganya [telling lies]
  49.  Usiwe kabaila                                  - Usichume tokana na jasho la mwingine [Don't exploit others]
  50. Usiwe kupe                                      -  Fanya kazi [be gainfully employed]
  51. Usiwe bwanyenye                             -  Usichume kwa vitega uchumi vyako [don't be a capitalist!]
  52. Usiwe na mrija                                  -  Usinyonye wenzako  [don't be exploitative]
  53. Utawala msonga                               - Utawala wa wachache [leadership of the few]
  54. Usiwe nyang'au                                 - Usidhulumu kwa kutumia madaraka [Don't use your position to exploit others]
  55. usiwe Kikaragosi                              -  Usiwe chui katika ngozi ya kondoo [Don't be a sheep in a leopard's skin]
  56. Umangimeza                                     -  Viongozi wanaopenda kuamrisha watu [a Dictatorship]
  57. Kutoa ya mwaka                               - Kufanya jambo zuri na la pekee [performing a unique act]
  58. Kumpa mtu ukweli wake                  -  Kumwambia mtu wazi [to be transparent]
  59. Pua kukaribiana kushikana na uso     -  Kukunja uso kwa hasira [to express anger]
  60. Sina hali                                            - Sijiwezi  [I am helpless (mostly when talking about love)]
  61. Kupiga uvivu                                     - Kukaa tu bila kazi [abject laziness]
  62. Kupiga kubwa                                   -  Kwenda moja kwa moja [vanishing act]
  63. Kumwekea mtu deko                         -   Kulipiza  kisasi [pay back]
  64. Mtu mwenye ndimi mbili                     -  Kigeugeu  [A turncoat]
  65. Miamba ya mitishamba                       - Wanga hodari wa kienyeji [ expert wizardry]
  66. Kupiga supu                                       - Tegea  [do the least]
  67. Kupiga mali shoka                              - Gawana  [distribute (contraband, bullion, inheritance]
  68. Kula vumbi                                         - Pata taabu   [struggle]
  69. Mafungulia ng'ombe                            - Kati ya saa mbili na saa tatu [between 8.00  and 9.00 o'clock
  70. Kutia kiraka                                        - Fichia siri [confiante]
  71. Kumlainisha mtu                                  -  Kumzungumzia mtu maneno matamu mpaka akubali matakwa yako [convince someone to see eye to eye - to agree to your argument]
  72.  

Mifano ya Nahau

NAHAU                MAANA
Kupiga moyo konde        kujituliza/kujiliwaza
Kujipa moyo       kujiliwaza
Kupiga hatua      kuendelea mbele
Kukata kamba   kuaga dunia
Kupiga darubini kufanya uchunguzi
Kutupa macho   kuangalia mbali
Kupigwa kalamu               kufutwa kazi
Kuandaa meza  kutayarisha chakula
Kugonga mwamba          kutofanikiwa
Kwenda msalani               kwenda chooni
Mifano ya Misemo

MSEMO               MAANA
Mkono wa birika              uchoyo
uzi na shindano ushirikiano
Shingo upande  bila kupenda
kiguu na njia       mtu asiyetulia mahali pamoja
Mdomo na pua karibu sana
Lila na fila             mema na mabaya

             

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]